Monday, March 18, 2013

Ni Ambassadors Christ kwenye Tamasha la Pasaka,utakuwa wapi?



KUNDI la muziki wa kiroho la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda linatarajia kuzindua albamu mpya iitwayo Kaeni Macho, Machi 31, mwaka kwenye Tamasha la Pasaka.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa kundi hilo limemhakikishia kwamba albamu hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali.
Alizitaja nyimbo zilizopo kuwa ni Kaeni Macho, Mungu Wangu, Tugireurukundo, Ewe Ndugu, Tuombeane, Umwamini Yesu, Msalaba, Twawona, Okuswala na Huruma.
“Kundi hilo maarufu kwa jina la Kwetu Pazuri, limefurahi sana kuja hapa Tanzania na wamenieleza albamu hiyo hawajawahi kuizindua hivyo ni baraka kubwa kwa Watanzania kupewa heshima hiyo,” alisema Msama na kuongeza kuwa kundi hilo pia litatumbuiza katika maonyesho mengine ya mikoani.
Kwa mujibu wa Msama hivi sasa kundi hilo linatamba na albamu ya Mtegemee Yesu na wamemhakikishia kuwa watang’arisha tamasha la mwaka huu na wamejipanga vya kutosha kuhakikisha mashabiki wanapata burudani ya nguvu.
Alisema albamu yao hiyo ina nyimbo nane ambazo ni JY’ Ushima Uwite, Mtegee Yesu, Ndifuza Kugerayo, Iyana Iby’ Isi, Yesu Niwe Mungeri, Parapanda, Abasaruzi na Nenda.
Licha ya kundi hilo, wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.
Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, Kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31, na litaendelea Aprili Mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora, Iringa, Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Tuesday, November 20, 2012

HUKUMU YA FUNDIKIRA WATU WALIA NA KUZIMIA MAHAKANI.


Leo ilikuwa ndiyo siku ya hukumu dhidi ya watuhumiwa watatu wa mauaji ya marehemu Swetu Fundikira aliyeuawa kwa kupigwa miaka miwili iliyopita. Mara baada ya watuhumiwa hao kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa, ndugu na jamaa wa marehemu waliangua kilio na wengine hadi kuzimia kama walivyoshuhudiwa na paparazi wetu aliyeweka kambi mahakamani hapo. Kushoto ni dada wa marehemu Rehema Fundikira, Hadija Mdemu shemeji wa marehemu.
....mmoja wa ndugu wa Fundikira akibebwa mara baada ya kuzimia na kudondoka sakafuni
....akipepewa huduma ya kwanza kwa kupepewa
....akipata nafuu kiasi
.....ndugu wakilia
ndugu wakilia
...ilikuwa ni saa ya majonzi na huzuni
Watuhumiwa wakiwa mahakamani kabla ya hukumu kusomwa. kutoka kulia ni Rhoda Robert, Ally Gube na Mohamed Ally.
...safari ya huzuni ya Rhoda Robert kuanza maisha mapya gerezani mara baada ya hukumu,

Wednesday, November 7, 2012

KANGA NA MISEMO YAKE





KANGA NA MISEMO YAKE




USILAUMU SISIMIZI SAUKARI HAIMALIZI,




UTAUMIZA ROHO YAKO,



SIRI NI YA WAWILI

KANGA KAMA TUNAVYOJUA NI VAZI LA MWANAMKE WA KITANZANIA KAMA ILIVYO




KITENGE, BATIKI,NA MAVAZI MBALIMBALI.



 UZURI WA VAZI HILI LA KANGA HUONGEZWA NA MISEMO ILIYO IBEBA KWANI MISEMO

HII MBALI YA KUBURUDISHA PIA INAFUNDISHA KAMA IKITUMIWA VIZURI.

HIVYO WANAWAKE TULIENZI VAZI LETU HILI NA SI KULIDHARAU ,

MPENDA KWAO HUTUNZWA LOLEST,



















OBAMA AWASHUKURU WAMAREKANI KWA KUMPA USHINDI


Michelle Obama akionyesha upendo kwa mumewe baada ya ushindi wake.

Obama akitoa hotuba baada ya ushindi wake leo huko Chicago.…

Michelle Obama akionyesha upendo kwa mumewe baada ya ushindi wake.

Obama akitoa hotuba baada ya ushindi wake leo huko Chicago.

Akiwa na mkewe, Michelle, na binti zake Sasha (wa pili kulia) na Malia Obama wakisherehekea ushindi wake.

Obama ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi, akiwa Ikulu ambako atakaa kwa miaka minne tena.

Familia nzima ya Obama ikifurahia ushindi.

Obama akitoa hotuba yake mbele ya umati wa watu huko Chicago.
Michelle Obama akiwa amepandwa ‘mzuka’ kwa ushindi wa Obama.
Mkutano wa Obama ulivyokuwa umepambwa kwa rangi mbalimbali za taifa hilo.
Mke wa Romney aitwaye Ann Romney, akimliwaza mumewe baada ya kushindwa.
Romney akiwashukuru waliompigia kura.
ALIYEKUWA mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, Barack Obama, amemshinda mpinzani wake kutoka chama cha Republican, Mitt Romney, katika uchaguzi uliofanyika jana.
Obama ambaye alishinda urais wa nchi hiyo miaka minne iliyopita, amesema hivi sasa ana dhamira ya hali ya juu zaidi na nguvu zaidi za kufanya kazi zake. Aliyasema hayo huko Chicago wakati wa hotuba yake ya kupokea ushindi huo.
Hata hivyo, wagombea wote wawili wa kinyang’anyiro hicho walitoa wito wa umoja kwa watu wa nchi hiyo kwa ajili ya maendeleo.
Katika hotuba hiyo alimshukuru mkewe na mabinti zake , Sasha na Malia, ambao alisema ni “wasichana wawili jasiri kama mama yao.”
Katika uchaguzi huo Obama alipata kura nyingi hususani katika majimbo ya Ohio, Iowa, Wisconsin, Pennsylvania, New Hampshire na Virginia.
Kiongozi huyo alipongezwa haraka na viongozi wengine duniani wakiwemo David Cameron wa Uingereza na Benjamin Netanyahu.

Tuesday, October 9, 2012

hivi ni baadhi tu, ya yaliyojiri ndani ya fiesta 2012,

Diamond na vijana wake wakivua nguo jukwaani wakati wa shoo ya Fiesta 2012.
...Wakizidi kuonyesha nguo zao za ndani.
Diamond akiwa stejini.
INAWEZEKANA kwamba Tamasha la Fiesta 2012, lilikumbwa na matukio mengi ya aibu lakini lile la mwanamuziki Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’, kuvua nguo na kumwaga ‘lazi’ mbele ya maelfu ya Watanzania, likawa la funga kazi kuliko yote.
Diamond ambaye alishangiliwa vilivyo, wakati akitumbuiza na kudhihirisha kwamba yeye bado moto wa kuotea mbali anapokabidhiwa jukwaa, alipozidiwa na mzuka, alisaula suruali yake na kubakiwa na kivazi cha ndani ambacho wengi hukiita ‘boxer’ (chupi).
Rick Ross akishusha burudani katika Fiesta 2012.
Mwanamuziki huyo, hakufanya hivyo peke yake, kwani aliposaula na wacheza shoo wake walimfanya vivyo hivyo, nao wakabakiwa na vi-boxer vyao.
Warembo wakipagawa na shoo ya Rick Ross 'The Boss'.
Hawakuishia hapo, baada ya kuvua na kubaki hivyo, wakawapa migongo mashabiki na kuwachezea, hivyo kukamilisha zoezi la kumwaga ‘lazi’.
BABY MADAHA NAYE
Uchunguzi unaonesha kwamba mwanamuziki Baby Madaha alikuwa msanii aliyetumia muda mwingi kujiandaa na shoo ya Fiesta 2012. Hata hivyo, jukwaa lilimkataa kutokana na mpangilio wa ratiba, kwa hiyo akabaki amejikunyata ‘back-stage’ wakati wasanii wenzake wakipanda jukwaani na kufanya kazi zao.
Baby Madaha akiwa katika pozi na jamaa.
Kwa upande mwingine, wasanii wa kiume walimuona kama ‘kiburudisho’ chao, kwani walipojisikia, walimvaa, wakamkumbatia na kumpiga mabusu.
Madaha katika pozi na Shetta.
Hili la kumkumbatia na kumpiga mabusu, lilichukuliwa kama ni la kumfariji lakini wengine hususan wanamuziki wa kiume, walisema wanaona burudani kumkumbatia na kumbusu.
KUNA WAREMBO WALITWANGANA
Gari aina ya Mercedes Benz, lililombeba mwanamuziki wa Kimarekani, Rick Ross, lilipoingia uwanjani, warembo wawili walijikuta wakiwashiana moto, kila mmoja akimsema mwenzake kuwa ana kiherehere.
Warembo hao, kila mmoja alikuwa anataka kulishika gari hilo kwa lengo la kumfikia Rick Ross ‘The Boss’ lakini katika kile ambacho wengi walikiona ni cha ghafla, wao kwa wao walishikana.
Hata hivyo, warembo hao waliamuliwa na kuondolewa uwanjani hapo, hivyo kuambulia sifuri, kwani siyo tu kwamba walishindwa kumfikia mwanamuziki huyo, bali pia hata shoo yake hawakuiona.
TATHMINI YA JUMLA
Fiesta 2012, limekuwa na mafanikio zaidi kutokana na kumshusha nchini msanii ambaye anakubalika zaidi ulimwenguni kwa kipindi hiki. Rick Ross, yupo kwenye orodha ya wanamuziki wa Hip Hop daraja la kwanza kwa sasa ndiyo maana ujio wake, umeweza kuongeza chachandu ya aina yake kwenye Fiesta. Lingine ni kwamba Diamond aliweza kuwavalisha nguo wanamuziki wake wa safu ya kuimba, kwani kabla hawajapanda, walionekana wakiwa hawana jipya.
Wanamuziki wa Hip Hop, waling’ara vizuri kwenye Fiesta ya mwaka huu.

Wednesday, October 3, 2012

HIVI NDIVYO BIRTHDAY YA DIAMOND ILIVYOKUWA NDANI YA D'MAGE HOTEL USIKU WA JANA

DIAMOND NA WASAFI.......
Kiukweli ntakua mchoyo wa fadhira endapo sintowashurukuru watu wote waliohudhuria katikaghafla fupi ya kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa iliyofanyika usiku wa jana 02/10/2012 katika hotel ya DEMAGE kinondoni...de Night was Crazy n Amazin , kiukweli nimefurahi sana kiasi kwamba hata sijui niwalipe kitu gani...
Hii ni cake maalum ambayo aliletewa  na Wema kama moja ya zawadi ya Birthday yake
Hapa akiwa na Dada yake wa hiyari Halima kimwana
Wema na dada yake Diamond Esma wakilishana Cake


mapenzi ni kikohazi kulicha huliwezi..........

All de way from UK Naj pia alikuwepo
Dimpoz kwa Poz, Mboni Masimba na Mecky




Hapa tukiwa na Roho ya Wolper Legraa Dallas

Bhaaaaaaasssssssss....!

Joff mnyama pia ndani
Hapa babtale na Naj wakiteta jambo

Team sheta pia Ndani....


Weeeeeeeeeeeeee.........!
Dallas tena......




gift from wema
 
 
 
Hapa wema na Mboni masimba
Kama ulikua haujui hawa ndio vijana wanaoongoza kwa Kuvimba mjini........LOL!








All de way from America Wasafi walikua ndani pia......

HAPPY BIRTHDAY DIAMOND












DOZEN & SHETTA
Watoto wa ManzeseTIPTOP pia ndani
Watuacheeeeee na Mama yangu mboni ali masimba.......