Friday, August 17, 2012

MAJEMBE MAPYA YA SIMBA,



KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amesema usajili wa wachezaji Daniel Akuffor raia wa Ghana na Paschal Ochieng (Kenya), utaleta mabadiliko katika kikosi chake kutokana na ubora wa wachezaji hao.
 Milovan, raia wa Serbia, alisema ameridhishwa na viwango vya wachezaji hao, ndiyo maana akatoa uamuzi wa kukubali waingie mkataba na timu hiyo.
“Nimeridhishwa na viwango vya wachezaji hawa, ndiyo maana nimekubali waingie mkataba na Simba. Wana viwango vizuri, nimewajaribu na nimeona wataweza kuisaidia timu katika upungufu uliojitokeza.
“Tunajiandaa vema kwa ajili ya msimu ujao na nina imani kiwango kitakachoonyeshwa na timu yangu kitakuwa ni cha hali ya juu, tutacheza mechi kadhaa za kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa ligi,” alisema Milovan

No comments:

Post a Comment